SIRI 5 ZAVUJA MAPIGANO NA MAGAIDI TANGA
STORI: Mwandishi Wetu/omary .j.sume
IMEBAINIKA! Mapambano
na wahalifu wanaosadikiwa ni magaidi kwenye Kitongoji cha Amboni jijini
Tanga, yameingia sura nyingine baada ya wakazi wa kitongoji hicho
kuvujisha siri tano, Amani limenyetishiwa.
Polisi wakiwa kwenye mapigano na wahalifu hao.
WALIKUWA NA WAPENZI
Kwa mujibu wa mkazi mmoja
wa eneo hilo, wahalifu hao walishakuwa na wanawake kwenye eneo hilo,
hivyo kama walikuwa na mpango wa kujua siri za Jiji la Tanga ilikuwa
rahisi sana.“Wale watu baadhi yao walikuwa na wanawake hapa Amboni. Na
hilo limebainika baada ya kutokea kwa mapambano na wao kukimbia kwani na
mmoja wao aliyekuwa na mwanamke hapa hajaonekana tena,” alisema mtoa
habari huyo.
WALIKUWA WAKICHENJI DOLA KILA BAADA YA SIKU MBILI
Habari kutoka kwa mkazi
mwingine zilidai kuwa, baadhi ya wahalifu hao walikuwa wakienda mjini
Tanga kila mara kwa shida ya kuchenji dola za Kimarekani.“Kuna wakati
nilikutana na watu wakisema wanatafuta maduka ya kuchenji dola za
Marekani, wakakosa na kwenda mjini. Nikawa nawaona mara kwa mara tena
wakienda mjini, nadhani ni kila baada ya siku mbili.
“Lakini
sikujua wanapoishi wala kazi zao. Naamini ni haohao maana baada ya
mapambano na wao sijawaona tena tangu Ijumaa iliyopita,” alisema mkazi
huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hans.
TABIA ZAO
Mjumbe wa nyumba kumi wa
kitongoji hicho, Idd Suleiman akizungumza na Amani alisema kuwa,
kulikuwa na watu walioonesha dalili kwamba si wenyeji wa eneo la
Amboni.“Mbaya zaidi, watu hawa walikuwa na tabia ya kuonekana nyakati za
usiku, kama ni mchana basi si kwa uwazi mkubwa. Nilijaribu kuwafuatilia
nikidhani ni wakazi wa mtaani kwangu lakini sikuwahi kuwajua,” alisema
mjumbe huyo.
Paul Chagonja.
WENGI WAO NI WAREFU, WEMBAMBA, WEUSI
Mjumbe huyo alizidi
kusema kuwa, watu hao waliokuwa wakionekana maeneo hayo ni wembamba,
wengine ni warefu na weusi lakini walionekana wakakamavu muda wote.
“Kusema kweli kama sisi
wananchi tungekuwa watafiti sana na kutoa taarifa polisi labda
wangekamatwa mapema kwani watu hao walikuwa hawafanani na sisi wakazi wa
eneo hili ambao tunajuana,” alisema.
NI KWELI WAMEKIMBILIA KENYA?
Naye mzee Juma Kabari
‘Mapipa’ yeye alisema kuwa, anavyojua miaka ya nyuma kuna Mzungu aliwahi
kumpoteza mbwa wake ndani ya mapango hayo.“Sasa katika kumtafuta
hakumpata, baadaye akaja kuonekana Mombasa nchini Kenya. Ikagundulika
kuwa, kuna pango moja ambalo linatokea Mombasa. Nina wasiwasi kwamba,
hata hawa jamaa (wahalifu), huenda walipita chini kwa chini wametokea
Mombasa, ndiyo maana hawajawakamata.
“Watu waliodaiwa kukamatwa juzi, siamini kama kweli ni miongoni mwa wale ambao walitoa upinzani kwa askari wetu Ijumaa iliyopita,” alisema mzee Mapipa.
Post a Comment