Header Ads

NDEGE AGEUKA MWANAMKE NIGERIA

Kisa cha kushangaza kilitokea nchini Nigeria
ambapo mwanamke mmoja alipewa kichapo
cha mbwa hadi akafariki kwa madai ya yeye
kuwa mchawi.
Mwanamke huyo inasemekana alikuwa Ndege
iliyokuwa inaruka mtini kabla ya kugeuka na
kuwa binadamu.
Umati wa watu ulikusanyika eneo alilokuwa
mwanamke huyo baahi wakinasa matukio
kwenye simu zao za mkononi. Polisi wawili
walilazimika kurusha mabomu ya petroli
kuwatawanya watu hao na kuwazuia kunasa
picha za mwanamke huyo aliyekuwa
anachapwa sana.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mmoja
alisema kuwa mwanamke huyo dakika chache
zilizopita alikuwa Ndege mtini kabla ya
kugeuka na kuwa mwanamke.
Ndege huyo alikuwa anazunguka mti mjini
Oshodi , kisha akagonga mlingoti wa stima
kabla ya kuanguka ardhini ambapo aligeuka
na kuwa mwanamke.
Hii ni kwa mujibu wa wakazi wa mjini Oshodi
wanaodai kuwa mwanamke huyo alikuwa
mchawi.
'Kitu cha kushangaza'
''Ni kitu cha kushangaza lakini ni cha kweli,''
alisema bwana Sobowale.
"tulipozungumza na mwanamke huyo alidai
kuwa na nguvu za kiganga, na kwamba
alikuwa amewaua watu kadhaa. Aliongeza
kuwa alikuwa anarejea kwa mumewe anayeishi
katika eneo la Mushin kabla ya tyukio hilo.
Baadhi ya watu walianza kumpiga picha. ''
Video ya umati huo ukimtandika mwanamke
huyo imeenea kama moto msituni na
kutazamwa na maelfu ya watu kwenye
mtandao wa kijamii wa YouTube.
Mwanamke huyo alikuwa uchi wa mnyama
huku ngozi yake ikiwa inatoka baada ya
kuchomwa.
Banke Idowu ni mmoja wa watu walionasa
video ya mwanamke huyo akiwa anachapwa
na umati na kwamba alikuwa amearifiwa na
wenzake kuhusu mwanamke huyo
alivyobadilika.
Aliambia BBC kuwa "sijawahi kuona jambo
kama hili maishani mwangu,lakini nimesikia
na kuona tu kwenye filamu kwa hivyo
waliponiambia kuwa limetokea , mimi
nimeamini. ''
Alisema angedhubutu kumuokoa mwanamke
huyo umati huo ungemgeukia na yeye.
Polisi hawajuzungumzia tukio hilo, hususan
kabla ya umati huo kukusanyika na kuanza
kumchapa mwanamke huyo.
Alifariki mda mfupi baadaye huku mwili wake
ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha hospitali kuu.
Samahani kwa picha tulizoweka

Hakuna maoni