Header Ads

MKURUGENZI WA KIKE KAMPUNI YA ULINZI YA SENGO AGONGANA NA BODA BODA

      Watu wakiendelea kufulika eneo la tukio
 Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sengo Security Gard ya mkoani hapa Mariam lsihaka Sengo akishuka kwenye gari lake baada ya kugongana na boda boda jioni hii eneo la Mji Mpya
  Mbele ni moja ya nyumba  zinazomilikiwa na kampuni hiyo ya Ulinzi.
 Mariam Sengo akihojiwa na mtandao huu muda mfupi uliopita
 
Kulia ni boda boda huyo akiwa chini ya ulinzi mkali wa wananchi,
hata hivyo boda boda huyo alifanikiwa kukimbia baada ya wenzake kufika eneo la tukio nakumtorosha kwa staili ya kujifanya kumpa pole na baadae kumpakia kwenye moja ya pikipiki na kutoweka naye kwa mwendo wa kasi.
 Mariam akifunga mlango wa gari lake
 Gari likiwa eneo la tukio
                Polisi wakiwasili la eneo la tukio
 Mariam akihojiwa na polisi



 Salim Sengo ambaye ni kaka wa Mariam akiikokota  pikipiki hiyo
 Pikipiki ikipelekwa kituo cha polisi
         Mariam akieleka kituo cha polisi.
                                       
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni maarufu ya Ulinzi mkoani Morogoro "Sengo Security Gard' Mariam Sengo jioni hii amepata ajari  baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na pikipik maeneo ya  Mji Mpya mkoani hapa.

Wakizungumzana mtandao huu baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema
" Huyu dada alikuwa akitokea mjini na nyuma yake kulikuwa na gari na kwamba alipofika hapa  aliwasha taa kuashiria anakata kulia na gari iliyokuwa nyuma yake ilipunguza mwendo boda boda huyu alikuja kasi na kutaka kuyapita magari yote mawili alifanikiwa kulipita moja na alipokaribia kulipita la pili alikuta tayari limeziba barabara likikata kona hivyo alikikuta akiligonga eneo la mrango na yeye kuanguka chini"alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Kobelo.

Boda boda huyo alikamatwa na  wananchi na kuwekwa chini ya ulinzi akitakiwa kusubiri serikali ifike ambapo kwamshanga wa wengi wenzake walifika eneo la tukio na kumtorosha kimtindo

Hakuna maoni