Zaidi 28 wauwawa na wanamgambo Kenya
Wanamgambo wa al-shabaab wanaaminika kutekeleza mauaji hayo.
Polisi
nchini Kenya wanasema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al
Shabaab wamewauwa kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 28 waliokuwa
wakisafiri kwenye basi moja karibu na mpaka wa Somalia.
Maafisa
wa ngazi ya juu wamesema kuwa basi hilo lilitekwanyara katika Jimbo la
Mandera wakati likiwa njiani kuelekea katika mji mkuu Nairobi.
Watu wasiokuwa waislamu wanasemakana kutengwa na abiria wengine na kisha kupigwa risasi.
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limetekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu mwaka 2011.BBC
Huo ndio mwaka ambapo Kenya iliwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kupigana na kundi hilo la waislamu wenye itikadi kali.
Mji wa
Mandera katika eneo la Kaskazini mashariki ndio ulioathirika pakubwa.
Baada ya shambulio hilo la mapema jumamosi maafisa katika eneo hilo
wamenukuliwa na vyombo vya habari nchini kenya wakisema kuwa serikali
ilikataa kuitikia ombi lao la kutaka usalama kudumishwa zaidi.
Afisa
mmoja ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba wavamizi hao waliwataka
abiria kusoma aya katika Koran kabla ya kuwaangamiza walioshindwa
kufanya hivyo
Post a Comment