Hivi ndivyo bangi inavyoingizwa katika magereza
BANGI ni dawa ya kulevya iliyopo kwenye kundi la dawa za kulevya lenye kuleta Njozi (Hellucinogences).
Vileta njozi huathiri ubongo na kumfanya mtumiaji kutoa tafsiri potofu ya hisia na kujisikia kama vile yuko nje ya dunia.
Mtumiaji wa bangi huzalishwa na kutumiwa kwa wingi barani Afrika kwa sababu hustawi maeneo mengi.
Nchini Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini, mkoani Njombe wilayani Makete hustawi zaidi.
Wakati Serikali ikiamini kuwa gerezani ni mahala salama hata kuwatunza wanaokamatwa na dawa za kulevya, hali si shwari katika baadhi ya magereza hapa nchini, kutokana na ongezeko la matumizi ya dawa hizo.
Baadhi ya askari Magereza, wafungwa na mahabusu katika magereza mbalimbali hapa nchini, wanahusishwa na biashara ya dawa za kulevya ndani ya magereza, imebainika.
Uchunguzi uliofanywa kwa miezi miwili sasa, umebaini kuwepo kwa dawa za kulevya katika magereza mengi hapa nchini, hususani Bangi.
Baadhi ya askari ambao hawakutaka kutajwa majina yao na vyeo katika Gereza la Ruanda na Songwe mkoani Mbeya, walithibitisha kuwepo kwa uingizwaji wa bidhaa hiyo ambayo inafanyika kwa siri kubwa katika magereza hayo.
Biashara hiyo inahusisha baadhi ya askari, wafungwa na mahabusu wenye kesi mbalimbali, wanaokaa muda mrefu gerezani huku kesi zao zikiahirishwa mara kwa mara.
Baadhi ya waliowahi kuwa mahabusu wa gereza la Ruanda mkoani Mbeya, wanaeleza kuwa wahusika wakubwa ni baadhi ya wafungwa wanaofanya kazi nje ya gereza, kisha kurejeshwa alasiri na baadhi wanaopelekwa mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi zinazowakabili.
Wanasema njia ambazo zinatumika kuingiza dawa hizo gerezani ni kujiingiza katika sehemu ya haja kubwa wakiwa nje ya gereza na wakati wa ukaguzi unapofanyika kwa kila anayeingia gerezani hapo, askari wanashindwa kubaini.
“Baadhi ya wafungwa ambao wanakaribia kumaliza muda wao, wanatolewa kwenda kufanya kazi za nje ikiwemo kwenda kukata nyasi za Ng’ombe na kurejeshwa mchana na wale wanaoenda kusaga mashine wanaweka kwenye unga. Hao wana mtandao na wauza bangi uraiani, wanaingia nazo na kufanya biashara ndani ya gereza, mle kuna biashara nyingi” anaeleza mmoja wa aliyekuwa mahabusu katika gereza hilo na kuachiliwa huru hivi karibuni baada ya Mahakama kuona hana hatia.
Baadhi ya askari mgambo wanaotumwa kuwachukua mahabusu na kuwapeleka katika mahakama za mwanzo, ambao nao waliomba hifadhi ya majina yao, walikiri kuwepo kwa biashara hiyo ambapo walisema kuwa, biashara hiyo inafanyika kutokana na vipato vidogo vya Mgambo na askari Magereza kutokuwa na mianya ya rushwa tofauti na askari polisi.
Mbali na bangi, wanasema kuwa, katika magereza pia kuna uvutaji mkubwa wa sigala ambazo huingizwa kwa njia za haja kubwa kisha kutolewa vyooni na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya sero na nje ya sero bustanini.
Wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, idara ya huduma za sayansi ya makosa ya jinai (GCRLA), inataja madhara yanayowakuta watu wanaotumia dawa hii ya kulevya kuwa ni kuwaza, kuona, kusikia na kuhisi vitu kwa namna tofauti au visivyokuwepo, kupata njozi, kuongezeka kwa hamu ya kula, kuwa kama kichaa, kutapika, wasiwasi, hamaki na kupumbaa.
Madhara yatokanayo na matumizi ya muda mrefu
Madhara hayo ni kupata ugonjwa wa akili, mabadiliko ya maono, hisia na mtizamo yasiyoisha, kuharibika kwa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kukumbuka na kufikiri na kukosa ari ya maendeleo na mabadiliko ya aina yoyote ile.
Sheria inasemaje kuhusu bangi
Kutumia, kuhamasisha matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifdhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na bangi ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha.

Mbali na tatizo la Bangi, moja ya matatizo yanayotajwa ni suala la kutumia kwa kubadilishana vitu vyenye ncha kali zikiwemo nyembe.
“Nilikamatwa na kupelekwa gerezani mwaka 2011, nikakuta watu wananyolea wembe mmoja ambapo kilichoniuma ni kwamba kuna rafiki yangu aitwaye Jack, alikuwa anaishi na VVU, alinyolea wembe akajikata, akampa jamaa anaitwa Kamugisha akajikata, naye akampa Side, naye akajikata na Side alimpa Chidi akatie kucha naye akajikata, virusi vikasambaa kwa wote”anasema Frank Kaitaba, kijana ambaye alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya Jijini Dar es Salaam na sasa anahudumiwa na shirika la Medecin De Munde la Temekelinalopunguza athari za madawa ya kulevya..
Anasema baada ya hapo akaamua kuwafuata madaktari wa gereza hilo na kuanzisha kikundi cha uelimishaji rika ndani ya gereza na kwamba tangu hapo ndani ya gereza hilo mtu anapotaka kunyoa anampa taarifa kiongozi aitwaye Onyango, ambaye anatoa wembe na kumwamuru nyapala asimamie matumizi ya nyembe. - See more at: http://www.jamiiforums.com/blog/riport-maalum-hivi-ndivyo-bangi-inavyoingizwa-katika-magereza/#sthash.Gzv9oOcg.dpuf

February 3rd, 2015 | by Gordon Kalulunga

Anasema baada ya hapo akaamua kuwafuata madaktari wa gereza hilo na kuanzisha kikundi cha uelimishaji rika ndani ya gereza na kwamba tangu hapo ndani ya gereza hilo mtu anapotaka kunyoa anampa taarifa kiongozi aitwaye Onyango, ambaye anatoa wembe na kumwamuru nyapala asimamie matumizi ya nyembe.

Post a Comment