SEMINA ELEKEZI KWA TANZANIA NZIMA
- Kuipa mafanikio makubwa Skauti
- Cheche za mabadiliko zazidi kuonekana
Harakati
za kuendeleza maendeleo ya kweli na kurudisha heshima ya Skauti kwa
jamii, harakati hizo zinazidi kukua na kuonekana zaidi, hii ni kufuatia
utekelezaji ulio na weledi kwa viongozi wa Chama cha Skauti na Maskauti
wote Tanzania.
Chama
cha Skauti Tanzania kimeandaa semina elekezi kwa makamishna wote
Tanzania, semina hiyo ya siku tatu kuanzia tarehe 18.02.2015 hadi
20.02.2015 inayoendelea katika ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar Es
Salaam.
Katika
mahojiano na Dar Scout Habari Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania
Mheshimiwa Abdulkarim Shah (Mb) alisema, ''Tumekutana kwa mujibu wa
taratibu zetu za Skauti, na kwakuwa toka tumeteuliwa hatujawai kukutana
na kufahamiana na pia kupanga mikakati ya pamoja katika kuhakikisha
kwamba Skauti inafanya kazi zile zinazotakiwa kwa mujibu ya Katiba yetu
na kanuni zake na pia kuisambaza Skauti nchini kote, isambae kwa manufaa
ya vizazi na nchi yetu''.
Mhe.
Shah (Mb) aliendelea kusema, ''Kukutana kwetu hapa, mada mbalimbali
zitatolewa na kupata fursa ya kuhoji na kutoa mawazo ambayo yote kwa
pamoja yatawekwa katika mkakati wetu wa miaka minne na tunaamini kwamba
kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake kwa mujibu wa taratibu za
Skauti'' aliendelea kusisitiza kwamba, ''Ili ndiyo kubwa kwa maana
mafunzo yatakayo tolewa hapa tunahitaji kila mmoja wao aende kwa nafasi yake akawajibike''.
Kamishna
Mkuu Mhe. Shah alieleza pia, viongozi hao watajengewa uwezo wa kufahamu
pale linapotokea jambo hatua gani ichukuliwe ya ziada na kila jambo
linalofanyika liweze kuratibiwa na kufika Makao Mkuu na kuwepo na
taarifa hizo, pamoja na Skauti kujua na kuwa na taarifa moja ya kila
jambo, kuanzia za kambi na nyinginezo. Hii ni faida kubwa ya utawala
bora.
Elasto
Nangati Kamishna wa Mkoa wa Mtwara alisema, ''Semina hii Elekezi
itawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ukizingatia hatujawai
kupewa semina elekezi kama hii kwa hiyo mabadiliko yatakuwepo sana baada
ya semina hii''. Aliendelea kusema kuwa, ''Lengo ni kuboresha utaratibu
wa uendeshaji, inamanufaa kwangu na kwa wenzangu, kwani itatujengea
uwezo sana wa kazi''
Kamishna Mkuu Msaidizi kitengo cha Miradi na Maendeleo Skauta Hamis Kerenge Masasa (aliyesimama) akiwaelekeza jambo wana semina. |
Katika
semina hii Skauti zaidi ya 112 wa jinsi zote walihudhuria, katika hali
iliyokuwa nzuri ya upendo na viongozi hao walionekana kuvalia sare za
kila aina na huku wakiwa na nyuso za furaha.
Kiongozi
kutoka Tanzania Zanzibar Skauta Makame Ali alisema, ''kulikuwa na vitu
ambapo tulikuwa kama kwenye giza kwa sasa tumefunuliwa na kujua mengi,
nami nitaenda kuwaelekeza wenzangu pindi nitakaporudi''.
Makamishna wakiwa katika kazi za vikundi katika Semina Elekezi |
Skauti walipata fursa ya kufundishwa mchezo wa CHESS |
Post a Comment