BIG SOO! MWANAJESHI ALEWA CHAKARI NA KULALA KATIKA MFEREJI WA MAJI MACHAFU MKOANI IRINGA!
KATIKA
hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT)
anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada
ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo
la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa.
Tukio hilo lilitokea muda
wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka
katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini
Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa
wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati
ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa
askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote
wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na
kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.
Hata
hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo
kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla
ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu.
Alisema
kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake
ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na
kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima
jeshi kwa ulevi uliopitiliza.
"Umelidhalilisha sana
jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare, sasa nataka kukuvua sare
kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi "
alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja.
Maamuzi hayo ya kiongozi
wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado
ni kijana mdogo sana maombi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza
katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa.
Ushauri wetu kwa askari
wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa
pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya
yako ama chonde chonde ulevi noma
Post a Comment