Header Ads

KESI YA SHEIKHE PONDA ISSA PONDA MAMBO BADO MAGUMU MOROGORO.

Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro (ODC) Zuberi Chembera (mwenye sale) akijaribu kuwazuia wafuasi wa katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda wasiisogelee gari iliyombeba wakati akirejeshwa gereza la mkoa baada ya kesi yake kughailishwa kwa kesi yake hadi januari 15/ 2015 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.PICHA/OMARY J. SUME

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda kushoto akizungumza jambo na mawakili wake, Juma Nasssoro na Bartholomew mara baada ya kughailishwa kwa kesi yake.PICHA/OMARY J.SUME
 

Wafuasi wa katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiangalia gari la polisi wakati likipita baada ya kesi yake kugailishwa.PICHA/OMARY J.SUME


Wafuasi wa katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wametanda barabara kuu ya Old Dar es Salaam wakati wakitoka mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro na kuelekea msikiti mkuu wa mkoa huo.
PICHA/OMARY J.SUME




KESI inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kislamu Shekh Ponda Issa Ponda,imeshindwa kusikilizwa huku mawakili wa pande mbili za mashtaka na utetezi zikivutana kuhusiana na mshtakiwa kupewa dhamana.
 
Kesi hiyo ambayo ipo mbele ya hakimu mwandamizi wa Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro Mary Moyo ilitajwa jana (Jumatatu) huku kukiwa na mabishano kuhusu kuanza rasmi kusikilizwa pamoja na mtuhumiwa kupewa dhamana.


Akiwasilisha hoja ya upande wa utetezi,wakili kiongozi Juma Nassoro aliwasilisha maombi matatu kwa mahakama hiyo kabla kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo .
Katika ombi lake la kwanza Wakili huyo alitaka kesi hiyo ianze kusikilizwa kwababu kwakuwa ukamilishaji wa taratibu za awali zilishakamilishwa kwa upande wa mashtaka na kumuomba hakimu kuipangia tarehe ya kuanza kusikilizwa na sio kutajwa.


Wakili huyo alisema kuwa kama kuna nyongeza au mabadiliko kwa upande wa mashtaka unaweza kufanyika huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa na kusisitiza kutoendelea kutajwa.


Katika ombi lake la pili,wakili huyo kiongozi alitaka mahakama kulifuta shtaka namba ambalo ni mshtakiwa kwenda kinyume na amri ya hakimu mkazi wa kisutu wa jijini Dar es Salaam iliyotolewa mei 9,2013 ambayo ilitoa adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kumtaka mshtakiwa asifanye jambo lolote la uvunjifu wa amani na badala yake ahubiri suala la amani.


Wakili huyo aliiambia Mahakama mshtakiwa alikata rufaa katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu hiyo ambapo katika hukumu iliyotolewa novemba 27 mwaka huu na jaji Augustine Shangwa alifuta hukumu ya mahakama ya kisutu ambalo ndio msingi wa shtaka namba moja ya kesi iliyopo katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro.


Wakili huyo mtetezi alisema kutokana na hukumu iliyotolewa na jaji Shangwa Mahakama hiyo kwahiyo shtaka namba moja halina uhalali hivyo mahakama inapaswa kuliondoa au kutoa muongozo.


Katika ombi lake la tatu wakili huyo aliambia Mahakama kuwa kutoka na mazingira yaliyobakia kwa sasaivi haki halisi na maslahi ya haki ya kimagakama yanatoa haki kwa mshtakiwa kupewa dhamana na hivyo kuiomba mahakama kuangalia haki ya mshtakiwa kupata dhamana kwa kuzingatia hukumu ya Jaji Shangwa .


Naye Wakili msomi anayemtetea mshtakiwa Bathoromew Tarimo,alisimama na kuuunga mkono hoja iliyosilishwa na wakili mwenzake huku akisisitiza kutokana na hukumu ya Jaji Shangwa hati ya mashtaka imebomoka pamoja na hati ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DDP)namba 148(4) cha mwenendo wa makosa ya jinai .


Alisema mteja wao yupo rumande tangu agosti 2013 licha ya upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi hivyo mshtakiwa anayo haki ya kupatiwa dhamana na kesi yake kuanza kusikilizwa.


Hata hivyo upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali kanda ya Mashariki

Benard Kongola akishirikiana na Wakili mwenzake Sunday Hyera walipinga mbele ya Mahakama hiyo maombi yote matatu.


Wakili Kongola alidai kuwa mahamuzi ya mahakama moja hayawezi kuingilia uhuru wa mahakama nyingine na kwamba hati ya mashtaka ipo moja na ina makosa matatu na kupinga kwamba haijabomoka.


Alisisitiza kesi iendelee kutajwa kwakuwa upande wa mashtaka wamechelewa kuipata hukumu ya jaji Shangwa ili waipitie na kuanza kuandaa mashahidi kwajili ya kutoa ushahidi wa kesi hiyo na kusema hoja ya upande wa utetezi haina mashiko.


Akitoa maamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili,Hakimu Moyo alisema hoja ziliwasilishwa na upande wa utetezi zina msingi,lakini anaungana na hoja zilizotolewa na upande mashtaka kwakuwa hata Mahakama hiyo haijapata nakala ya hukumu ya jaji Shangwa licha ya upande wa utetezi kumkabidhi nakala muda mchache kabla ya kesi hiyo kuanza.


Hakimu Moyo alisema anapaswa kuipitia kwa kina hukumu hiyo ili kuwa muongozo wa uendeshaji wa kesi hiyo na kukubalina na hoja ya upande wa mashtaka kesi hiyo iendelee kutajwa huku mshtakiwa akiendelea kubaki rumande na kesi hiyo imepangwa kutajwa tena januari 5,2015.


Shekh Ponda alifunguliwa kesi namba 128/2013 katika Mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo aliyatenda Agosti 10 mwaka 2013 katika eneo la Kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro na alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 19 mwaka 2013

Hakuna maoni