POLISI FFU ADAIWA KUBAKA MTOTO
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida askari polisi mmoja wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU) mkoani Shinyanga anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato
cha kwanza mwenye umri wa miaka 13 (Jina limehifadhiwa) na kumsababishia
maumivu makali.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mama mdogo anayeishi na mwanafunzi huyo polisi
huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Alex alitenda kitendo hicho saa
nane usiku wa kuamkia juzi huko Ngokolo Manispaa ya Shinyanga baada ya
kumkamata kwa nguvu alipokuwa akitokea chooni kujisaidia na kumwingiza
chumbani kwake.
Mama
huyo alisema mara baada ya kumwingiza chumbani huku akiwa amemziba
mdomo kumzuia asipige kelele, alimvua nguo zake za ndani na kuanza
kumwingilia kwa nguvu na alipokidhi haja zake alimruhusu kutoka katika
chumba hicho na kumtisha kwamba iwapo atamweleza mtu yeyote atamfanyia
kitu kibaya ambacho hatakisahau maishani mwake.
“Juzi
usiku mnamo saa 8:00 nilisikia mlango ukifunguliwa, nilitoka chumbani
kwangu na kwenda kuangalia sebuleni anapolala mwanangu ili kuona ana
tatizo gani, sikumkuta sehemu hiyo anayolala, nilihisi ameenda uani
kujisaidia na kweli baada ya muda kama robo saa hivi nilimsikia
akirudi.”
“Nilitoka
na kumuuliza alipokuwa amekwenda akajibu kwa upole alikuwa ameenda
kujisaidia, sikumdadisi sana nilirudi chumbani kwangu na nikaendelea
kulala, asubuhi kulipopambazuka pia hakuna jambo lolote alilonieleza,
nilienda kwenye shughuli zangu na nilirudi nyumbani mchana na kumkuta
hayuko katika hali ya kawaida,” alieleza mama huyo.
Alisema
hata alipomchunguza alibaini hata kutembea kwake ilikuwa ni kwa shida
na ndipo alipomketisha chini kumtaka amweleza kinachomsumbua iwapo
anaumwa aseme ili apelekwe hospitali kutibiwa na baada ya kusitasita kwa
muda aliamua kueleza ukweli wote kwamba alibakwa na polisi huyo ambaye
pia anapanga katika nyumba wanayoishi.
“Kwa
kweli aliponipa taarifa hiyo nilisikitika sana, nilichukua hatua ya
kumsubiri huyo polisi atoke kazini ambapo nilimuuliza kwa nini
alimfanyia mwanangu kitendo kiovu, mwanzo alisita kukubali, lakini
baadae alikiri na kusema alikuwa amepitiwa na kujikuta akimfanyia
kitendo hicho.”
“Hata
hivyo alinishangaza baada ya kunihoji kwamba baada ya kufanya hivyo
mimi nataka nini, sikuridhishwa na majibu yake, nilitoka na kwenda
kumwalifu mchungaji wa kanisa letu ili aweze kunisaidia juu ya hatua za
kumchukulia polisi huyo, alipokuja aliamua pia tuwaarifu watu wa Agape
ili waweze kutusaidia kupata msaada wa kisheria,” alieleza.
Mama
huyo alisema baada ya kuwasiliana na watu wa Shirika la Agape
waliongozana pamoja na mtoto aliyebakwa hadi katika kituo cha polisi
ambako walipewa fomu namba tatu kwa ajili ya kwenda hospitali kupimwa na
baadaye walirejea kituoni na mtoto huyo alimtambua mtu aliyembaka na
kutoa maelezo katika dawati la jinsia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba atatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha
uchunguzi ambao tayari unaendelea kufanyika.
SOMA HABARI ZAIDI
Post a Comment