MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA ARUSHA
Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja ayetajwa kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini Arusha akiwa na mama yake.
Mtoto
wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota
wa Sokoni One jijini hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa
eneo hilo.Tukio
hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo
anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama
yake usiku wa manane.
Akizungumza
na paparazi wetu, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja
la Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa
jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda
kwenye kikundi cha akina mama.
Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye
anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa,
nikarejea nyumbani.“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa
kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia nirudi nyumbani
nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya,
aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa
narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa
na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.“Niliamua
kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri
zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi
mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali,
alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa
shilingi laki moja,” alisema mama huyo.
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada
ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa
akimtibu kwa kutumia miti shamba.Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo
cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya
kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za majirani ndipo
alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika
nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia
hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya
Mount Meru ambako anatibiwa.
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano
Post a Comment